Habari za Mchana rafiki zangu
Napenda kuwakaribisha kwenye blog hii,hapa tunajadili aina
za vyakula ambavyo hutumika kama tiba mbadala kwa magonjwa ambayo tunakumbana
nayo katika maisha ya kila siku.
Mfululizo wa mwangaza huu ambao nimeona nitumie na rafiki
zangu utakuwa kama mwanzo wa maisha mapya maana kwa kiwango kikubwa tafiti
zimeonyesha ni kwa jinsi gani mlo mzuri na uliokamilika (balanced Diet)
huchangia kwa asilimia sitini(60%) katika kurefusha maisha hasa kwa kikazi hiki
tulichonacho.
Leo nitapenda kuongelea chakula au vyakula ambavyo hushauriwa kutumiwa mahususi kwa kujenga kiungo muhimu kwa binadamu kijulikanacho kama Moyo.
Moyo ni kiungo katika mwili ambacho huduma yake kwetu ni kubwa na hivyo huitaji uangalizi wenye mapenzi ya dhati na kuujali kwa kiwango cha hali ya juu,leo nimeanda aina mbili ya vyakula na kinywaji ambacho hupaswa kusaidia kuboresha na kujenga Moyo bila kusahau kuuepusha na magonjwa kama Presha n.k
Mchemsho wa Mbogamboga (Mixed Vegetables)
MAHITAJI
-250g ya Njegere(peas) au Green Beans
-500g ya Aubergine
-250g ya Carrots
-100g ya Maharage Soya
-400g ya Viazi Mviringo
-01 Kitunguu
-02 Tangawizi
MAANDALIZI
-Hakikisha kimeoshwa vyema tayari kwa kupikwa
-Menya kama itakuwa ni njegere au maharage ya kijani vyema
-Kisha katakata Aubergine vipande vidogo vidogo kisha kwa ziada unaweza nyunyizia limao kuleta ladha
-Kisha chemsha kwa muda wa dakika thelathini(dk 30)
Mlo huu husaidia kuongeza madini na vitamini kwenye moyo.
Pia chakula hiki hushauriwa kwa watu wenye matatizo ya
Arterial Hypertension- kwa kuwa mchanganyiko huu wa mboga una kiwango kikubwa cha Potassiamu na pia Sodium katika kiwango cha chini hivyo kusaidia kuzuia Presha ya kupanda (High Blood Pressure) pia uhamasisha uzalishaji wa uchafu maji(diuresis- Urine Production)
Imeandaliwa
Dr Naomi J.K Mdongo
Presented by
Millan Abraham.
Bon Appertite
No comments:
Post a Comment